Loading...

Nay wa Mitego: Tarajieni ngoma nyingine kubwa na Diamond

Nay wa Mitego amedai kuwa nyimbo za ushirikiano kati yake na Diamond hazijafika kikomo. Amedai kuwa wawili hao wanajiandaa kuja na ngoma nyingine – kubwa.

“Kwa muda huu kidogo tunatoa gap, tutarudi na ngoma kubwa ya pamoja na tukiangalia mazingira ya album kuuzika basi tutaachia album ya pamoja mimi na Chibu,” Nay alimwambia mtangazaji wa kipindi cha SayariBit cha Pambazuko FM ya Ifakara, Morogoro, Keneth Ngamoga.
Nay alikuwa Ifarakara kwaajili ya show.
Kuhusu kutofanyika video ya wimbo wao Mapenzi au Pesa, Nay alisema ni kutokana na wote wawili kuwa na ratiba ngumu na zinazotofautiana.
Nay na Diamond walifanya vizuri na wimbo wao Muziki Gani.

Source: Bongo5

Video: Diamond Platnumz Ft. Rayvanny Salome ( Traditional )

Msanii Diamond Platnumz ameamua kuachia video mpya ya wimbo ‘Salome’ amemshirikisha Rayvanny, Video imefanyika hapahapa Tanzania, imeongozwa na Director Nicorux kutoka South Africa.

Saad Lamjarred wa Morocco, ni mwanamuziki mkubwa kuzidi Davido, Wizkid au Diamond

Kimuziki, Afrika Kaskazini imejitenga na nchi zingine za Afrika, Kusini, Mashariki na Magharibi.
Image result for saad lamjarred

Kutokana na hilo, tumejikuta tukishindwa kuwafahamu wasanii wakubwa wa nchi kama Morocco, Misri, Algeria na kwingine. Mfano, Saad Lamjarred ni msanii mkubwa wa Morocco, ambaye namba zake zinatisha – ni balaa kabisa!
Kwanza ana followers milioni 3.5 Instagram. Hiyo inafuta kile tulichokuwa tunaamini kuwa, Davido ndiye mwanamuziki wa Afrika mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao huo (2.9m) akifuatiwa na Diamond (2.7m) huku Wizkid akiwa na 2.5m.



Video yake mpya, GHALTANA ilitoka August 25, lakini hadi sasa imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 36. Kama hiyo haitoshi, video ya wimbo wake, LM3ALLEM iliyotoka May 2, 2015 ina zaidi ya views milioni 390.
LM3ALLEM uliingia kwenye kitabu cha Guinness World Record kwa kupata views milioni 100 ndani ya miezi mitatu. Ni video ya kiarabu iliyotazamwa kuliko zote.
Image result for saad lamjarred lm3allem
Nyimbo zake “Mal Habibi Malou” na “Machi Sahel” zimevutia views milioni 161 na milioni 66 kwenye Youtube hadi sasa.
Source: Bongo5

Picha: Raymond aonyesha mjengo anaoishi na gari analotumia

Ndoto ya wasanii wengi ni kupata maisha bora, nyumba mzuri pamoja na magari ya kifahari. Mkali wa wimbo ‘Natafuta Kiki’ Raymond ‘Rayvanny’ ameonyesha mafanikio aliyopata ndani ya muda mfupi.
Nyumbani kwa Rayvany WCB

Muimbaji huyo ambaye anajiandaa kwenda kwenye show nchini Burundi akiwa na wasanii wenzake wa WCB, ameonyesha nyumba anayoishi na gari ambalo atalitumia kwa sasa.
“Daaah! eti namimi leo naingia kwangu, kweli Mungu hana upendeleo,” Rayvanny aliandika ujumbe huu instagram katika hiyo picha hapo juu.
Toka Rayvanny ajiunge na WCB, ameshafanya nyimbo mbili, ‘Kwetu’ pamoja na ‘Natafuta Kiki’ ambazo zimpatimia mafanikio makubwa kwa muda mfupi.

Source: Bongo5

Video: Kijana apoteza ulimi kwa kung'atwa wakati wakinyonyana ndimi na mwanamke.

Kijana Said Mamba (24) mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, amelazwa hospitali baada ya kung’atwa sehemu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.


Mamba ambaye kwa sasa hawezi kuzungumza, aling’atwa Septemba 12, saa 3:30 usiku wa kumkia Sikukuu ya Idd el Hajj.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.
“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.
Source: Bongo5

Mtangazaji mpya wa Clouds FM, Kicheko ni jiwe lililogeuka dhahabu

Maisha ni safari na hatutakiwi kukata tamaa kwa kuwa hatujui kesho yetu. Ukiisikia historia ya maisha ya mchekeshaji ambaye kwa sasa amegeuka kuwa mtangazaji wa Clouds FM, Kicheko unaweza kutokwa na machozi kama huna uvumilivu.

Awali Kicheko alikuwa member wa Ze Comedy ya EATV baada ya kuchaguliwa kwenye shindano la kutafuta wasanii watakaogiza kwenye kipindi hicho ambapo alidumu hapo kwa muda wa miaka isiyopungua miwili.
Waswahili wanasema “acha kazi, uone kazi, kupata kazi, ilivyokuwa kazi,” lakini kwa Kicheko haikuwa ngumu kwake kuacha kazi EATV ya uchekeshaji baada ya kuchukua maamuzi ya kuandika barua ya kuacha kazi kwenye uongozi wa kampuni hiyo April, 2014 huku akiwa hana kazi. Lakini pia mtangazaji huyo amepinga taarifa za kuwa alifukuzwa kazi kwenye kituo hicho cha runinga.
Baada ya muda kupita Kicheko alifanikiwa kupata shavu la utangazaji kwenye redio ya EFM akiendesha kipindi cha Singeli ‘Genge’ ambacho kimekuwa kikipendwa zaidi na mashabiki mitaani na kufanya brand yake kuanza kuwa kubwa.
Kumbe ilikuwa ni dhahabu huku wengi wakidhani lilikuwa ni jiwe, rangi yake ilifichwa na vumbi ndiyo maana kila mpita njia alilidharau kabla ya EFM na hatimaye Clouds FM kuliokota jiwe hilo na kulisafisha na hatimaye sasa rangi yake halisi imeonekana na kila mtu ameanza kulitamani tena.
Akikaribishwa kwa mara ya kwanza leo kwenye ofisi za Clouds Media (mjengoni) kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ mtangazaji huyo ameelezea historia yake kidogo huku akidai kuwa aliwahi kuwa mwizi huko nyuma. “Mwanzo nilikuwa mwizi, mkabaji. Unajua haya ni maisha tu,” amesema Kicheko.
Kwa sasa Kicheko amepewa heshima kubwa na watu wa mtaani ikiwa ni pamoja na kumpa jina la ‘Rais wa Uswazi’ kutokana na support yake anayoitoa kwenye muziki wa Singeli ambao umeonekana kukubalika zaidi kwa sasa huku akiwa na wanachama 489 kwenye kikundi chake.
Mchekeshaji huyo anatarajiwa kuanza kazi kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uswazi Flava’ hapo Clouds FM.
Source: Bongo5
© Copyright Daily News | Designed By beld
Back To Top